KIONGOZI WA UPINZANI KOREA KUSINI ACHOMWA KISU MBELE YA WAANDISHI WA HABARI

Category : International | Sub Category : Politics Posted on 2024-01-02 12:52:12


KIONGOZI WA UPINZANI KOREA KUSINI ACHOMWA KISU MBELE YA WAANDISHI WA HABARI

SEOUL

Kiongozi wa upinzani nchini Korea Kusini, Lee Jae-myung (59) amechomwa kisu akiwa kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari katika Mji wa Busan, asubuhi ya leo Jumanne January 02,2024. 

Lee ambaye alikosa nafasi ya Urais wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Urais mwaka 2022, amechomwa kisu upande wa kushoto wa shingo yake ambapo Mtu aliyemchoma  kisu anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 50 hadi 60 na amekamatwa katika eneo la tukio.

Kwa sasa Lee amepelekwa Hospitali akiwa katika hali mbaya ambapo ripoti zinasema kabla ya kumchoma kisu Mtu huyo alikuwa amemkaribia Lee ili kumuomba saini yake. 

Picha na video zinazoonesha shambulio hilo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha Lee akianguka katikati ya mkusanyiko wa Watu, wakati baadhi ya Watu wakijaribu kumkamata Mshambuliaji ambapo picha na video za tukio hilo zimegusa hisia za wengi mitandaoni. 

Lee ambaye ni Kiongozi wa Chama cha Democratic Party of Korea, kwa sasa sio Mbunge lakini anatarajiwa kuwania uongozi katika uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika mwezi Aprili 2024.

Online streaming
Search
Leave a Comment: